• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 16-March 22)

    (GMT+08:00) 2019-03-22 20:05:10

    Maonesho ya mafanikio ya jeshi la China kulinda amani ya dunia yaanza kwenye makao makuu ya AU

    Maonesho kuhusu kazi na mafanikio ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China PLA kwenye ulinzi wa amani duniani na kuhimiza maendeleo ya pamoja, yamezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

    Maonesho hayo ya siku tano yameandaliwa na mamlaka za China, yakiwa na picha zinazoonesha jinsi jeshi la China linavyohimiza amani ya dunia na maendeleo ya pamoja.

    Kwenye ufunguzi wa maonesho hayo konsela mkuu wa ubalozi wa China kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika Bw. Chen Xufeng amesema siku zote jeshi la China limekuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya dunia, jambo linalojenga sura ya China ya kulinda amani ya dunia, kuhimiza maendeleo ya dunia na kusimamia utaratibu wa kimataifa.

    Ofisa mkuu wa maswala ya amani na usalama wa Umoja wa Afrika Bw. Admore Kambudzi ameshukuru uungaji mkono wa China kwa Afrika kwenye maeneo mbalimbali, na kusema ushirikiano kati ya pande hizo mbili unaendelea kukua siku hadi siku.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako