• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 23-March 29)

  (GMT+08:00) 2019-03-29 20:03:15

  Kampuni ya Boeing yashtakiwa kwa ajali ya Shirika la Ndege la Ethiopia

  Kampuni ya utengenezaji ndege ya Boeing imefunguliwa mashtaka nchini Marekani na familia ya moja ya abiria waliofariki kwenye ajali ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

  Watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walifariki katika ajali hiyo iliyotokea mapaema mwezi huu.

  Ndugu wa Jackson Musoni, ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa na raia pekee wa Rwanda aliyekuwemo kwenye ajali hiyo, wanadai kuwa ndege sampuli ya Boeing 737 Max zinamapungufu ya kiusanifu katika mifumo yake ya kujiendesha. Ndege zote 371 zinazomilikiwa na mashirika mbalimbali za aina ya 737 Max zimepigwa marufuku kuruka toka ilipotokea ajali hiyo, ambayo ilikuwa ni ya pili kwa sampuli hiyo ndani ya miezi mitano. Ajali ya kwanza ilitokea mwezi Oktoba 2018 nchini Ethiopia na kuua watu wote 181 waliokuwamo ndani.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako