• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 23-March 29)

  (GMT+08:00) 2019-03-29 20:03:15

  MCT, asasi nyingine zashinda kesi dhidi ya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 dhidi ya serikali

  Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imesema baadhi ya vipengele katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inakiuka uhuru wa kujieleza pia vinapingana na Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao Tanzania imeuridhia.

  Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa hukumu alhamisi wiki hii dhidi ya sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 2, 2016 na kusainiwa na Rais John Magufuli.

  Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2017 ilifunguliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wakilalamikia ukandamizaji wa uhuru wa habari. Vipengele vilivyolalamikiwa vipo 18, walalamikaji wakiiomba mahakama hiyo itamke kwamba vipengele hivyo vinakiuka mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuilazimisha serikali kuvifuta kabisa.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako