Papa Francis asema kuzuia watu kubusu pete yake ni suala la kiafya na si vinginevyo
Papa Francis amevunja kimya chake juu ya mkasa wa kuzuia waumini kubusu pete yake akisema lilikuwa ni suala la kiafya zaidi.
Msemaji wa Vatican Alessandro Gisotti amesema kuwa Papa alikuwa akihofia kusambaa kwa vijidudu alipokuwa akikutana na waumini wa Kanisa Katoliki siku ya Jumatano.
Wahafidhina ndani ya kanisa walipinga vikali kitendo hicho wakidai Papa anavunja utamaduni wa muda mrefu wa kanisa. Gisotti amesema kuwa kulikuwa na watu wengi waliokuwa kwenye msururu wa kumsalimia Papa na yeye akawa na tahadhari juu ya uwezekano wa kusambaza vijidudu.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mwenye miaka 82 anadaiwa "kufurahishwa" na utata huo, msaidizi wa Papa amewaambia waandishi wa habari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |