• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 6-July 12)

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:54:33
  Wakimbizi wa Burundi Tanzania wasema 'wametishiwa kurudishwa nyumbani'

  Wakimbizi kutoka Burundi katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania ijumaa wiki hii walilalamika kuwa maafisa wasimamizi katika eneo hilo wamewatishia kuwarudisha kwa lazima nyumbani.

  Wakimbizi hao walisema hawatokuwa salama iwapo watarudishwa Burundi.

  Hata hivyo serikali ya Tanzania imekana kuwa kuna mpango wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyo karibu na mpaka na Burundi. Wakimbizi hao wameeleza kwamba mkuu wa kambi hiyo, Jumanne Singani, aliwataka warudi kwa hiari kabla ya kushurutishwa kurudi nchini humo. Zaidi ya wakimbizi 200,000 wa Burundi wanaishia Tanzania, wengi wao wakiwa wametoroka ghasia nchini mwao zilizozuka mnamo 2015.

  Mwaka jana Serikali ya Tanzania ilisema kuwa inajiondoa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa yanayowahifadhi.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako