• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 6-July 12)

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:54:33

  Serikali ya kenya yaondoa vibali ya makampuni ya kubeti

  Serikali ya Kenya imefuta kwa muda vibali vya makampuni takriban 27 ya mchezo wa bahati nasibu hadi yatakapolipa ushuru.

  Hii inakuja karibu zaidi ya mwezi mmoja baada ya kikosi cha maafisa kutoka mashirika mbali mbali kufanya uchunguzi wa leseni za makampuni yote ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya. Katika taarifa iliyotolewa Jumatano na Mkurugenzi wa Bodi ya Udhibiti na utoaji wa Leseni ya michezo ya Bahati nasibu nchini Kenya, Liti Wambua pia imeagiza makampuni yote ya simu za mkononi yenye huduma za huduma za kutuma na kupokea pesa kubatilisha nambari za makampuni hayo za pay bill zinazotumiwa na kampuni zilizoathiriwa na hatua hiyo.

  Tayari wachezaji wa michezo ya bahati nasibu wameanza kupokea ujumbe unaoonyesha kuwa kuna tatizo kwenye mtandao wa mchezo.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako