• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 6-July 12)

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:54:33

  Nicki Minaj ajitoa kwenye tamasha Saudi Arabia baada ya kukosolewa

  Mwanamuziki Nicki Minaj amelazimika kuvunja tamasha alotakiwa kulifanya nchini Saudi Arabia wiki ijayo akisema anaunga mkono haki za wanawake na wapenzi wa jinsia moja.

  Taarifa za nyota huyo wa miondoko ya rap kutumbuiza Saudia ziliwashtua wengi na kusababisha kelele kali kutoka kwa wanaharakati wanaokosoa rekodi ya haki za binadamu ya nchi hiyo.

  Wengine wakawa wanajiuliza msanii huyo atavaaje kwenye tamasha hilo kwa kuwa nchi hiyo inafuata mfumo wa kihafidhina wa Kiislamu, na Minaj ni maarufu kwa kuvaa nusu uchi. Saudi Arabia imekuwa ikijaribu kulegeza vikwazo kwenye sekta ya burudani ili kukuza sekta ya sanaa kwa ujumla ya nchi hiyo. Ukoselewaji wa Saudia kwenye eneo la haki za binadamu uliongezeka zaidi baada ya mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki mwezi Oktoba mwaka jana.

  Mwezi Machi mwaka huu, nchi hiyo ikaingia lawamani zaidi baada ya kuwafungulia mashtaka wanawake 10 ambao ni wanaharakati wa haki za binaadamu.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako