• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 6-July 12)

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:54:33

  Mwanamke aishi na maiti ya mamake nyumbani tangu 2016

  Mwanamke mmoja jimboni Texas, Marekani amekamatwa baada ya masalio ya maiti ya mamake inayooza kugunduliwa nyumbani wanakoishi pamoja.

  Polisi wanaamini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 71 alianguka mnamo 2016.

  Wanatuhumu kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 47 alishindwa kumhudumia vizuri mamake aliyefariki "siku chache baadaye" kutokana na athari ya kuanguka huko.

  Masalio ya mwili wa marehemu yalipatikana kwenye sakafu ya chumba kimoja. Binti yake na mjukuu wake marehemu walilala katika chumba cha pili katika nyumba hiyo. Mjukuu wa marehemu alikuwa na miaka 15 wakati akiishi na maiti ya bibi yake. Na kutokana na hilo, mamake ameshtakiwa kwa 'kumdhuru mtoto' wa chini ya miaka 15.

  Mjukuu huyo sasa anatazamwa na jamaa zao na anapokea usaidizi kutoka kitengo cha kuwalinda watoto.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako