• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 10-August17)

    (GMT+08:00) 2019-08-16 18:31:53

    Ndege zisizo na rubani za Uturuki zaanza kazi kaskazini mwa Syria wakati maandalizi ya eneo salama yanaendelea

    Ndege zisizo na rubani za Uturuki zimeanza operesheni kaskazini mwa Syria ambako eneo salama litaanzishwa kwa mujibu wa makubaliano kati ya nchi hiyo na Marekani.

    Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema juhudi zinafanyika ili kuanzisha Kituo cha Operesheni cha Pamoja katika mkoa wa San li urfa, kusini mashariki mwa Uturuki mapema iwezekanavyo.

    Wiki hii Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema ujumbe wa Marekani wenye watu sita umewasili nchini humo ili kujiandaa kwa uzinduzi wa Kituo cha Operesheni za Pamoja unaotarajiwa kufanyika katika eneo salama linalotarajiwa kuanzishwa nchini Syria siku kadhaa zijazo.

    Wiki iliyopita, maofisa wa kijeshi wa Uturuki na Marekani walikubaliana kuratibu na kusimamia eneo hilo kaskazini mwa Syria, hatua inayoonekana kupunguza uwekezano wa uvamizi wa kijeshi wa Uturuki.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako