• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 10-August17)

    (GMT+08:00) 2019-08-16 18:31:53

    Vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege wa Hong Kong zalainiwa

    Msemaji wa ofisi ya Hong Kong na Macao ya baraza la serikali la China Bi. Xu Luying amekasirishwa na kulaani vikali vitendo vya wahuni kuwapiga waandishi wa habari na watalii wa China bara kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong na kuunga mkono polisi wa Hong Kong kuwakamata wahuni hao kwa mujibu wa sheria.

    Nayo Ofisi ya serikali kuu katika mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong imetoa taarifa ikilaani vikali vurugu zilizofanywa na wahuni ikiwemo kuwapiga watu wawili wa China bara na kuwakamata, na kusisitiza kuwa siku zote ofisi hiyo inasaidia wahusika kuhakikisha usalama na maslahi ya watu wa China bara katika Hong Kong, na kuunga mkono polisi wa Hong Kong kuwakamata wahalifu hao mapema iwezekanavyo kwa mujibu sheria.

    Awali wiki hii mamlaka ya viwanja vya ndege katika mkoa wenye utawala maalum wa Hongkong, China imetangaza kusitisha huduma zote za safari za ndege baada ya uwanja huo kuzidiwa na waandamanaji.

    Mamlaka hiyo imewataka abiria waondoke kwenye uwanja huo haraka iwezekanavyo, na kutoa wito kwa watu mashuhuri kuepuka kwenda kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hongkong. Aidha, Kituo cha Dharura katika uwanja huo kimefunguliwa.

    Ofisa mkuu wa Mkoa wa Hong Kong Bibi Carrie Lam Cheng Yuet-ngor wiki hii amesema, watu walioandamana mkoani Hongkong wiki iliyopita, walipuuza sheria na kushambulia maofisa wa usalama wakiwemo polisi, ili kutimiza lengo la kuharibu utawala wa sheria. Amesema utawala wa sheria ni kiini muhimu kwa Hongkong, lakini hivi sasa jamii ya mkoa huo imeingia kwenye mvutano mkubwa, , na itahitaji muda mrefu kurejea hali ya kawaida.

    Bi. Carrie Lam Cheng Yuet-ngor ameeleza wasiwasi wake mkubwa kutokana na hali iliyotokea mkoani Hongkong wiki iliyopita. Matukio makubwa ya uharibifu yakiwemo kufunga njia ya reli chini ya bahari na ile juu ya ardhi, hali iliyoathiri vibaya wakazi wanaoenda kazini, pia tarehe 12, Uwanja wa Kimataifa wa Hongkong uliathiriwa vibaya na waandamanaji jambo lililolazimu ni kusitisha kazi. Waandamanaji walishambulia vituo vya polisi, na kuwashambulia maafisa wa polisi kwa silaha na kuwatupia mabomu ya petroli.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako