• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 14-Machi 20)

  (GMT+08:00) 2020-03-20 19:16:55

  Leo ni siku ya maombi Kenya:

  Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza taifa la Kenya kwa maombi maalum hii leo ili kuombea taifa wakati huu linapokumbwa na tishio la virusi vya corona. Akitoa agizo hili mapema wiki hii, rais aliwasihi wakenya kutumia fursa hii kuomba na kupiga dua kwa Mwenyezi Mungu kuinusuru Kenya na dunia nzima.

  Wakenya wataombea majumbanbi mwao kwani maikutano yote ya hadhara imepigwa marufuku.

  Huku hayo yakijiri, serikali ya Kenya itaanza mikakati ya kuwapima wakenya virusi vya corona kuanzia leo. Watu wanaoishi maeneo ambayo waathiriwa wanatoka ndio watakaopewa kipao mbele kwenye shughuli hii. Wakenya wameombwa kushirikiana na serikali.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako