• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 14-Machi 20)

  (GMT+08:00) 2020-03-20 19:16:55

  China: Shughuli zaanza kurejea upya, tangu kuibuka kwa janga la Corona

  Shughuli zimeanza kurudi kama kawaida nchini China, katika ishara kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona. Migahawa imeanza kufunguliwa huku idadi ya watu wakikusanyika tena katika mabustani, hiyo yote ikionyesha ishara kuwa China inaibuka na ushindi katika vita vyake dhidi ya virusi vya Corona ambavyo vimeutikisa ulimwengu.

  Kwa wakati huu, China imeweka mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo kwa kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa na pia kupima viwango vya joto mwilini kwa watu wanaoingia katika maeneo ya umma.

  Pia migahawa imeweka sheria za kuwazuia watu kukaribiana wanapokula ndani ya migahawa hiyo. Mikakati yote hiyo, licha ya ugumu wake katika utekelezaji lakini inaonekana kuwa na manufaa.

  Sehemu kubwa ya nchi hiyo sasa imeondoa vikwazo na watu wameanza kurudi kazini, tofauti na nchi za magharibi ambapo serikali zimeanzisha marufuku ya usafiri.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako