• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 22-Agosti 28)

    (GMT+08:00) 2020-08-28 15:34:56

    Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa anamatumaini janga la corona litakomeshwa ndani ya miaka miwili.

    Akizungumza mjini Geneva, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema homa ya Spanish flu ya mwaka 1918 ilichukua miaka miwili kudhibitiwa.

    Lakini ameongeza kuwa kuimarika kwa teknolojia ya sasa huenda haenda ikasaidia ulimwengu kudhibiti virusi ndani ya "muda mfupi".

    Mafua ya mwaka 1918 yaliwaua watu karibu milioni 50 duniani.

    Coronavirus kufikia sasa imewaua karibu watu 800,000 na wengine karibu milioni 23 kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo

    Dkt Tedros pia alijibu maswali kuhusu ufisadi unaohusishwa na vifaa ya kinga binafsi (PPE) wakati wa janga la corona, na kutaja ufisadi huo kama "uhalifu".

    Japo swali linaohusiana na ufisadi liliangazia zaidi Afrika Kusini, nchi kadhaa zinakabiliwa na suala hilo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako