Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya njaa na utapiamlo Afrika Mashariki
Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) limesema kuwa njaa kubwa na utapiamlo vinawakabili mamilioni ya wakimbizi walioko mashariki mwa Afrika mashariki wanaoishi kwa kutegemeamsaada kutoka kwa shirika hilo la chakula.
Limesema kuwa athari za kijamii na kiuchumi za janga Covid-19 zimepunguza msaada muhimu kutoka kwa wahisani.
WFP tayari liimepunguza usambazaji wa chakula au utoaji wa pesa kwa kiwango cha hadi 30% kwa zaidi ya wakimbizi milioni 2.7 waliopo katika mataifa ya Ethiopia, Uganda, Kenya, Sudan Kusini, na Djibouti, limesema.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |