• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 12-Septemba 18)

    (GMT+08:00) 2020-09-18 16:48:13
    Mafuriko makubwa yasababisha watu 217,000 kupoteza makazi nchini Ethiopia

    Waziri wa amani wa Ethiopia Bw. Muferiat Kamil, amesema watu karibu 217,000 wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miaka 30 iliyopita nchini Ethiopia.

    Bw. Kamil amesema katika maeneo kadhaa mafuriko hayo yalikuwa makubwa kabisa katika karne moja iliyopita na yamesababisha watu 217,000 kupoteza makazi yao na wengine 363,000 kuathiriwa vibaya. Majimbo matano yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko hayo ni Gambella, Kusini, Afar, Oromia na Amhara.

    Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuwa watu milioni 15.1 nchini Ethiopia wanahitaji msaada wa chakula kutokana na athari za mafuriko, janga la COVID-19, nzige wa jangwani na maafa mengine yanayosababishwa na binadamu. OCHA inasema inahitaji dola za kimarekani bilioni 1.44 kukidhi mahitaji ya kibinadamu nchini Ethiopia, lakini mpaka sasa bado haijapata fedha za kutosha kuendeleza operesheni zake.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  11  12  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako