Kampuni ya Huawei nchini Kenya imezindua programu ya mwaka huu ya watu wenye vipaji vya Tehama, yenye lengo la kuendeleza vipaji vya watu wenye ujuzi wa Tehama wakati uhusiano kati ya China na Kenya ukiendelea kuimarika.
Mkuu wa kampuni ya Huawei nchini Kenya Bw. Will Meng, amesema kwa mara ya kwanza programu hiyo itaendeshwa kwa njia ya kidigitali na kutoa mafunzo ya siku tano kwa washiriki 60 watakaojifunza kuhusu teknolojia ya 5G, Big Data, Akili bandia na Cloud Computing, ili kuwawezesha kuelewa mwelekeo wa sasa wa teknolojia hizo.
Program hiyo ni sehemu ya mpango wa wajibu kwa jamii wa kampuni ya Huawei, wenye lengo la kuendeleza vipaji vya Tehama na kuhimiza ujenzi wa kikanda wa jumuiya ya kidigitali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |