• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 12-Septemba 18)

    (GMT+08:00) 2020-09-18 16:48:13

    Kenya yafungua anga yake kwa Tanzania wakati maambukizi ya COVID-19 yakiwa yamepungua

    Jumatano wiki hii Serikali ya Kenya iliiongeza Tanzania kwenye orodha ya nchi zinazoweza kuanzisha huduma ya usafiri wa ndege za kimataifa kwenda kwenye nchi hiyo, na kumaliza mvutano wa kidiplomasia kuhusu usafiri wa ndege uliodumu kwa wiki kadhaa.

    Mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya iliiongeza Tanzania na nchi nyingine tisa kwenye orodha ya nchi ambazo watu wake hawatahitaji kukaa kwenye karantini kwa siku 14 baada ya kufika Kenya.

    Kufuatia uamuzi huo wa Kenya mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania ilitangaza kuondoa zuio la ndege za Kenya kwenda nchini Tanzania. Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Hamza Johari amesema uamuzi huo utaanza kutekelezwa mara moja na mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya tayari imearifiwa.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  11  12  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako