• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 12-Septemba 18)

    (GMT+08:00) 2020-09-18 16:48:13
    Wanafunzi 10 wafariki katika ajali ya moto uliotokea shuleni kaskazini magharibi mwa Tanzania

    Wanafunzi 10 wamefariki na wengine 7 kujeruhiwa baada ya moto kuunguza bweni moja katika shule ya msingi ya wavulana iliyoko katika kijiji cha Itera, wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, kaskazini magharini mwa Tanzania.

    Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia jenerali Marco Gaguti amesema, wanafunzi watatu kati ya saba waliojeruhiwa hali zao ni mbaya. Amesema moto huo ulitokea jana usiku saa tano kwa saa za huko, na kuunguza bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 74. Ameongeza kuwa, wanafunzi wengi waliokwama ndani ya bweni hilo waliokolewa na polisi, kikosi cha uokoaji, na watu wanaoishi jirani na shule hiyo.

    Mkuu huyo wa mkoa alisema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, lakini ameunda kamati ya uchunguzi, ambayo anatumai kuwa itagundua chanzo cha moto huo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  11  12  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako