• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 12-Septemba 18)

    (GMT+08:00) 2020-09-18 16:48:13
    Ethiopia imerekodi wakimbizi wa ndani milioni 1.8 katika mwaka huu

    Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) inasema hadi sasa Ethiopia ina wakimbizi wa ndani (IDPs) zaidi ya milioni 1.8.

    Ripoti hiyo ina takwimu zilizokusanywa kati ya mwezi Juni na Julai kwenye maeneo 1,200 yanayohifadhi wakimbizi wa ndani na kwenye vijiji zaidi ya 1,200 vinavyotajwa kuwa watu hao wamerudi. Chanzo kikuu cha watu hao kuwa wakimbizi wa ndani ni migogoro iliyochangia asilimia 68 ya watu hao kukimbia makazi yao, na vyanzo vingine ni ukame na mafuriko.

    IOM imesema itaendelea kufanya ufuatiliaji wa uhamiaji wa wakimbizi hao ili iweze kutoa takwimu zenye usahihi kwa serikali kuu, serikali za majimbo na serikali za mitaa ili kuwafuatilia watu hao.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  11  12  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako