Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Miaka 30 ya mageuzi ya sekta ya uchapishaji nchini China
  •  2008/11/20
    Tokea China ilipokumbwa na uhaba wa vitabu mpaka kuwa nchi mgeni muhimu itakayoshiriki kwenye maonesho hayo makubwa ya vitabu duniani, hali hii imedhihirisha wazi kwamba China imepata maendeleo makubwa katika mageuzi ya sekta ya uchapishaji katika miaka 30 iliyopita.
  • "Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mwaka 2008" lastawisha maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika
  •  2008/11/14
    "Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mwaka 2008" ambalo pia ni maingiliano makubwa ya kiutamaduni kati ya China na Afrika lilifanyika mjini Shenzhen China kuanzia tarehe 23 Oktoba mpaka tarehe 2 Novemba. Wasanii na wataalamu wa Afrika na China wana matumaini kuwa China na Afrika zitaimarisha zaidi urafiki wa jadi na kukuza zaidi maingiliano hayo na kupanua maelewano kwa njia nyingi zaidi.
  • Tamasha la Michezo ya Sanaa la Asia
  •  2008/11/06
    Tamasha la 10 la Sanaa la Asia lilifungwa hivi karibuni katika mji wa Kaifeng mkoani Henan, China. Kauli mbiu ya tamasha hilo ni "Upatanifu wa Asia na Kukutana kwa Furaha Mkoani Henan". Maonesho ya aina mbalimbali na shughuli nyingi za utamaduni za umma ziliufanya mkoa huo kuwa kama bahari ya furaha.
  • Mabadiliko makubwa yametokea katika maingiliano ya kiutamaduni na nchi za nje katika miaka 30 iliyopita
  •  2008/10/23
    Miaka 30 imepita tokea China ifungue mlango kiuchumi. Katika miaka hiyo, maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na nchi za nje yamepelekea mabadiliko makubwa kutoka maingiliano ya kiraia hadi ya kiserikali na hivi sasa yameingia katika kipindi cha kufana.
  • Msanii wa kuchora picha kwenye gamba la yai
  •  2008/09/25
    Kuchora picha kwenye gamba la yai ni sanaa ya jadi nchini China. Sanaa hiyo licha ya kuwapendeza Wachina pia inawavutia sana watalii wa nchi za nje ambao wananunua mayai hayo na kurudi nayo nyumbani.
  • Maonesho ya utamaduni wa China katika kipindi cha Michezo ya Olimpiki ya Beijing wavutia wageni
  •  2008/09/18
    Michezo ya Olimpiki ya 29 ilifanyika mjini Beijing kuanzia tarehe 8 Agosti mpaka tarehe 24. Michezo hiyo licha ya kuwa ni tamasha kubwa la mashindano pia ni jukwaa la kuwaoneshea wageni waliotoka kila pembe ya dunia utamaduni wa China unaog'ara.
  • Kwaya ya Kenya "Kayamba Africa" itakuja China
  •  2008/07/17
    Mwishoni mwa mwezi Julai makundi saba ya nyimbo na ngoma kutoka Afrika yataonesha michezo yao yenye jina la "Usiku wa Afrika" kwenye Jumba la mikutano ya Umma la Beijing yakichangia shamrashamra za Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Moja ya makundi hayo ni kwaya ya Kenya "Kayamba Afrika".
  • Hali ya zamani na ya leo ya sanaa ya picha za Puhui za mwaka mpya wa jadi wa China
  •  2008/07/10
    Sanaa ya picha za Puhui za mwaka mpya wa jadi wa China katika mji wa Gaomi mkoani Shandong imekuwa na historia ya miaka zaidi ya 500. Sanaa hiyo ilipita vipindi tofauti vya ustawi, picha hizo ziliwahi kuwa bidhaa zilizonunuliwa sana lakini baadaye hali ya sanaa hiyo ilididimia. Katika miaka ya hivi karibuni, wasanii wa picha hizo wameifufua sanaa hiyo kwa kufanya juhudi nyingi
  • Filamu ya "Mali za Urithi za Dunia Nchini China" yaanza kuoneshwa
  •  2008/07/03
    Wakati Michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, filamu ya "Mali za Urithi za Dunia Nchini China" imeanza kuoneshwa. Hii ni filamu ya kwanza inayoeleza kirefu mali za urithi wa mabaki ya utamaduni na sehemu za asili nchini China.
  • Msanii wa utamaduni wa jadi Zhang Hai
  •  2008/06/26
    Msanii Zhang Hai wa kabila la Wadong wilayani Sanjiang katika mkoa wa Guangxi, kusini mwa China ni mwanamuziki na mtengenezaji hodari wa ala ya muziki ya kikabila iitwayo lusheng ambayo amejifunza mwenyewe. Alitembeatembea katika vijiji vingi wanakoishi Wadong kurithisha ufundi wake wa kutengeneza ala hiyo.
  • Mpiga piano maarufu wa China Li Jian
  •  2008/06/05
    Bw. Li Jian alizaliwa miaka 43 iliyopita katika familia ya wanamuziki mjini Shanghai China, yeye ni pandikizi la mtu mwenye mikono mikubwa na nguvu. Ingawa si mtu hodari kwa kuongea, lakini anapozungumzia muziki wa piano maneno yake hayaishi.
  • Mwigizaji mashuhuri wa China Pu Cunxin
  •  2008/05/18
    Bw. Pu Cunxin ni mwigizaji wa China ambaye licha ya kuwa anajulikana sana kutokana na michezo yake ya kuigiza, pia ni mwigizaji mashuhuri katika filamu na michezo ya televisheni, kadhalika pia ni mwenezi wa ujuzi wa kinga dhidi ya UKIMWI.
  • Nyimbo anazoimba Han Lei
  •  2008/05/01
    Mwimbaji Bw. Han Lei alizaliwa mjini Beijing, alianza kujifunza kupiga tarumbeta (trombo), na kuanzia hapo alianza kujihusisha muziki maishani mwake. Mwaka 1999 alishiriki kwenye "mashindano ya waimbaji chipukizi" na aliwavutia wasikilizaji kwa sauti yake.
  • Biashara iliyostawi katika mji wa kupigia filamu na televisheni nchini China
  •  2008/04/03
    Katika miaka ya hivi karibui filamu zilizopigwa chini ya mwongoza filamu maarufu wa China Bw. Zhang Yimou zimekuwa zinajulikana duniani kutokana na filamu alioongoza, hasa filamu za "Shujaa" na "Curse of the Golden Flower". Watazamaji wa filamu hizo walivutiwa na mazingira ya mapambano makali, lakini mazingira hayo yote yalipigwa katika mji wa Hendian wa kupigia filamu na televisheni nchini China
  • Mpiga fidla maarufu wa China Lin Zhaoliang
  •  2008/03/27
    Hivi karibuni mpiga fidla maarufu wa China Lin Zhaoliang alifanya maonesho hapa Beijing. Muziki wake aliopiga kwa fidla yake uliwavutia sana watazamaji.
  • Mwimbaji wa China Zheng Xulan
  •  2008/03/10
    Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita China ilipoanza kufanya mageuzi ya kiuchumi mwimbaji Bi. Zheng Xulan aliishangaza China nzima kutokana na mtindo wake tofauti wa uimbaji wa nyimbo kwa sauti yake nyororo.
  • Mwimbaji mlemavu Liang Fuping
  •  2008/02/25
    Katika mji wa mlimani Chongqing, kusini magharibi mwa China, yupo mwimbaji mmoja anayejulikana kote mjini humo, ambaye si mmahiri wa kuimba tu bali pia ni mtungaji nyimbo. Kutokana na ulemavu wa mguu wa kulia, inampasa abebe gitaa mgogoni na kutembea kwa bakora.
  • Mila na desturi za mwaka mpya wa jadi wa China
  •  2008/02/11
    Kwa mujibu wa kalenda ya kilimo ya China tarehe 7 Februari ni sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina, yaani sikukuu ya Spring. Kwa Wachina siku hiyo ni muhimu sana, sherehe yake inaanzia leo na kuendelea kwa siku 15.
  • Biashara ya haki ya kunakili iliyofana nchini China
  •  2008/01/28
    Kwenye tamasha la vitabu lililofanyika hivi karibuni mjini Beijing, biashara ya haki ya kunakili ilifana sana. Kwenye tamasha hilo wachapishaji kutoka nchini na nchi za nje walipata fursa nzuri ya kufanya ushirikiano na biashara ya haki ya kunakili.
  • Filamu za kusherehekea mwaka mpya zaoneshwa kila mahali nchini China
  •  2008/01/07
    Filamu hizo zilizopigwa kwa nia ya kuchangia furaha ya mwaka mpya, zilianza kuoneshwa miaka kumi iliyopita. Tokea mwaka 1997 filamu za kuchekesha na kuoneshwa katika siku za mwaka mpya zimepigwa nyingi zikiwa ni pamoja na filamu za "Upande wa A na B katika Mkataba wa Kibiashara", "Simu ya Mkononi" na "Hakuna Mwizi Duniani", lakini mwaka huu filamu zinazooneshwa katika siku za mwaka mpya
  • Maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na nchi za nje kwa mwaka 2007 yalikuwa mengi
  •  2007/12/24
    Tarehe 21 Novemba"Wiki ya Filamu ya Sri Lanka" ilianza mjini Beijing. Tofauti na filamu za Ulaya, filamu za Sri Lanka ni za aina nyingine kabisa ambazo zinawavutia watazamaji wa China kwa kuonesha mila na desturi na maisha ya kidini ya watu wa Sri Lanka.
  • Tamasha la nane la maonesho ya sanaa la China laonesha mafanikio mapya ya utunzi wa michezo ya sanaa
  •  2007/12/10
    Kuanzia tarehe 5 Novemba kwenye majumba zaidi ya 30 katika miji 6 mkoani Hubei, vikundi vya wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini China vinaonesha michezo yao na kugombea "tuzo ya Wenhua" ambayo ni tuzo ya ngazi ya juu kabisa kati ya tuzo za michezo ya sanaa nchini China
  • Mihadhara ya Profesa Yu Dan yavutia jamii
  •  2007/11/26
    Wachina wa leo wanauchukuliaje utamaduni wao wa jadi? Ilikuwa saa tano za usiku, muda mfupi baada ya wageni wa Bw. Xiao kuondoka na jamaa zake wakiwa tayari kulala baada ya kupanga panga nyumba, lakini wakati huo Bw. Xiao aliwasha televisheni bila kujali akihimizwa na jamaa zake "lala basi!"
  • Wachoraji ndugu wawili Zhou
  •  2007/11/12
    Ndugu wawili Zhou ni wachoraji mashuhuri duniani, mtindo wao wenye uvumbuzi wa kijasiri, uchoraji wao wa picha, ufinyanzi wa sanamu na uchongaji picha kwenye mbao unawavutia na kuwastaajabisha sana watazamaji.
  • Mfasiri na mshairi Shu Cai
  •  2007/10/22
    Hivi karibuni, mshairi wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 83 Bw. Yves Bonnefoy alipata tuzo kubwa ya Franz Kafka ya fasihi ya Ulaya kwa mwaka 2007. Habari hiyo ilimfurahisha sana mshairi wa China Bw. Shu Cai, kwa sababu katika miaka mingi iliyopita aliwafahamisha wasomaji wa China kuhusu mshairi huyo, tuzo hiyo inathibitisha kuwa yeye hakukosea kuchagua mwandishi aliye hodari na kufasiri vitabu vyake.
  • Mpiga piano mashuhuri wa China Yin Chengzong
  •  2007/10/08
    Mpiga piano mashuhuri wa China Bw. Yin Chengzong ana umri wa miwaka 66, alipokuwa na umri wa miaka kumi na zaidi aliwahi kupata tuzo katika mashindano ya kimataifa ya muziki wa piano. Katika miaka ya 50 na 60 alianza kuwajulisha wakazi wa kawaida muziki wa Kimagharibi na huku akianza kupiga muziki wa Kichina kwa piano.
  • Maonesho ya kimataifa ya vitabu mjini Beijing
  •  2007/09/24
    Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu mwaka 2007 mjini Beijing yalimalizika hivi karibuni kwa mafanikio makubwa, wachapishaji kutoka nchini na nchi za nje walikuwa na pilikapilika nyingi wakati wa maonesho hayo.
  • Mwongozaji wa filamu wa Hong Kong Bw. Chen Kexin
  •  2007/09/10
    Bw. Chen Kexin ni mwongozaji wa filamu wa Hong Kong aliyepata tuzo mara nyingi zaidi, yeye pia ni mwongozaji wa filamu aliyegundua na kuwasaidia sana waongozaji filamu vijana barani Asia.
  • Tamasha la kimataifa la washairi lafanyika nchini China
  •  2007/08/27
    Tamasha la kwanza la kimataifa la washairi limefungwa hivi karibuni kwenye Ziwa Qinghai, ziwa ambalo lipo kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet, kaskazini magharibi mwa China. Katika tamasha hilo washairi kutoka nchi 34 wakiwa pamoja na washairi wa China, walighani mashairi yanye mada ya "Binadamu na Maumbile, Dunia Yenye Mapatano".
  • Mpiga piano msichana Li Ang
  •  2007/08/13
    Mpiga piano msichana Li Ang ana umri wa miaka 22, siku za karibuni kwa mara ya kwanza alifanya maonesho ya muziki wa piano mjini Beijing.
    1 2 3