Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Mwongozaji wa filamu za hifadhi ya mazingira Bw. Feng Xiaoning
  •  2008/10/30
    Mwezi Oktoba filamu ya "Kimbunga Kikali" imekuwa ikioneshwa kila mahali nchini China. Filamu hiyo iliyogharimu Yuan milioni 50 katika matengenezo yake inagusa hisia za watazamaji kwa nguvu. Inafahamika kwamba filamu hiyo imechaguliwa kuwa mojawapo ya filamu zinazooneshwa katika Tamasha la 21 la Kimataifa la Filamu mjini Tokyo.
  • Mwongozaji mkuu wa sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Beijing Bw. Zhang Jigang
  •  2008/09/18
    Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ilifunguliwa Tarehe 6 Septemba, sherehe ya ufunguzi huo iligusa hisia za watu na kuwapa picha nzuri zisizosahauliwa. Mliosikia ni wimbo uitwao "Kwenye eneo la mbinguni" ulioimbwa na mwimbaji mlemavu asiyeweza kuona Bw. Yang Haitao. Mwimbaji huyo alipoimba wimbo huo, ndege aliyemithilisha mwangaza wa jua akiruka angani na kutua kwenye ardhi ya majani,
  • Mwongozaji mkuu katika kuandaa sherehe za ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing Bw. Zhang Yimou
  •  2008/09/11
    Sherehe kubwa na ya kushangaza dunia nzima iliyofanyika tarehe 8 Agosti katika ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing na sherehe iliyojaa furaha na nderemo iliyofanyika tarehe 24 Agosti katika ufungaji wa michezo hiyo, sherehe hizo mbili zote ziliwapa watu kumbukumbu zisizosahaulika. Mwongozaji mkuu katika kuandaa sherehe hizo ni Bw. Zhang Yimou.
  • Mwigizaji kijana wa mchezo wa opera ya kunqu Kunqu ya China Bw. Yu Jiulin
  •  2008/06/12
    Mchezo wa opera ya kunqu Kunqu ambayo hadi sasa imekuwa na historia ya miaka zaidi ya 600 inasifiwa kama ni chimbuko la aina zote za opera za jadi nchini China, ni sanaa iliyoorodheshwa na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO katika urithi wa utamaduni usioonekana duniani
  • Mwimbaji maarufu wa Tibet bibi Cedai Drolma
  •  2008/05/12
    Bibi Cedai Drolma alizaliwa mwaka 1937 kwenye familia moja maskini ya wakulima watumwa. Miaka zaidi ya 50 iliyopita, Tibet ilikuwa inatekeleza mfumo wa wakulima watumwa, na asilimia zaidi ya 95 ya watibet walikuwa watumwa. Wakati huo masufii wa ngazi ya juu na makabaila wachache walikuwa wanamiliki mali zote za Tibet, na hata wakulima watumwa pia ni mali yao ya binafasi
  • Mwigizaji mwanamke wa China Chen Xiaoyi
  •  2008/03/17
    Chen Xiaoyi ni mwigizaji mwanamke ambaye katika miaka ya hivi karibuni amekuwa anaonekana mara kwa mara kwenye televisheni kutokana na michezo yake ya kuigiza kuoneshwa, yeye ni mwigizaji wa Jumba la Michezo ya Kuigiza la Beijing.
  • Wakulima wajitahidi kustawisha biashara ya utamaduni ili kuondoa umaskini
  •  2007/12/03
    Qinghai ni mkoa wenye wakazi wa makabila mengi, raslimali za utamaduni wa kikabila ni nyingi. Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya mkoa imekuwa inajaribu kuwawezesha wafugaji kuongeza mapato yao kwa njia ya kustaswisha biashara katika sekta ya utamaduni wa kikabila
  • Mtunzi mashuhuri wa muziki Guo Wenjing
  •  2007/11/19
    Bw. Guo Wenjing ni mtunzi mashuhuri wa muziki nchini China, gazeti la New York Times lilisema, "yeye ni mtunzi pekee wa muziki nchini China aliyepata heshima kubwa duniani ambaye hakuwahi kuishi kwa muda mrefukatika nchi za nje". Muziki wake unapigwa katika matamasha mengi ya kimataifa ya muziki.
  • Mwigizaji nyota wa filamu Li Lianjie (Jet Lee)
  •  2007/10/29
    Bw. Li Lianjie anayejulikana kwa wengi kama Jet Lee, mwenye umri wa miaka 44, ni mwigizaji mashuhuri wa filamu za gongfu. Tokea mwaka 1982 alipoigiza filamu yake ya kwanza ya "Hekalu la Shaolin", hadi sasa ameigiza filamu 33 za michezo ya gonfu. Hivi karibuni filamu yake ya "Shujaa Huo Yuanjia" ilioneshwa mjini Beijing.
  • Mfasiri na mshairi Shu Cai
  •  2007/10/22
    Hivi karibuni, mshairi wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 83 Bw. Yves Bonnefoy alipata tuzo kubwa ya Franz Kafka ya fasihi ya Ulaya kwa mwaka 2007. Habari hiyo ilimfurahisha sana mshairi wa China Bw. Shu Cai, kwa sababu katika miaka mingi iliyopita aliwafahamisha wasomaji wa China kuhusu mshairi huyo, tuzo hiyo inathibitisha kuwa yeye hakukosea kuchagua mwandishi aliye hodari na kufasiri vitabu vyake.
  • Mpiga piano mashuhuri wa China Yin Chengzong
  •  2007/10/08
    Mpiga piano mashuhuri wa China Bw. Yin Chengzong ana umri wa miwaka 66, alipokuwa na umri wa miaka kumi na zaidi aliwahi kupata tuzo katika mashindano ya kimataifa ya muziki wa piano. Katika miaka ya 50 na 60 alianza kuwajulisha wakazi wa kawaida muziki wa Kimagharibi na huku akianza kupiga muziki wa Kichina kwa piano.
  • Mwongozaji wa filamu wa Hong Kong Bw. Chen Kexin
  •  2007/09/10
    Bw. Chen Kexin ni mwongozaji wa filamu wa Hong Kong aliyepata tuzo mara nyingi zaidi, yeye pia ni mwongozaji wa filamu aliyegundua na kuwasaidia sana waongozaji filamu vijana barani Asia.
  • Mwandishi wa vitabu ambaye pia ni askari polisi, Cao Naiqian
  •  2007/07/30
    Bw. Cao Naiqian mwenye umri wa miaka 59 ni askari polisi katika mji wa Datong mkoani Shanxi. Lakini tofauti na askari polisi wengine, yeye pia ni mwandishi mashuhuri wa vitabu. Vitabu vyake zaidi ya 30 vimetafsiriwa kwa lugha za kigeni na kusambazwa katika nchi za Japani, Marekani, Canada na Uswis.
  • Mcheza Filamu Mwanamke Yu Feihong
  •  2007/07/16
    Yu Feihong ni mcheza filamu nyota nchini China, ingawa yeye bado ni kijana na jina lake linavuma sana miongoni mwa watazamaji, lakini anaishi kimya na kawaida kabisa.
  • Li Yuchun mwanafunzi wa kike aliyejulikana ghafla na kuwa maarufu
  •  2007/07/09
    Mwaka 2005 kipindi cha "mashindano ya kuchagua wanafunzi hodari wa kike" kilichotangazwa na kituo cha televisheni cha Mkoa wa Hunan kiliwavutia watu wengi nchini China, na mwanachuo Li Yuchun aliyeshinda kwenye mashindano hayo akapendwa na vijana wengi wa kike na wa kiume nchini China.
    1 2 3 4