Hekalu la Jidu 2006/07/17 Hekalu la Jidu lililoko katika mji wa Jiyuan mkoani Henan ni hekalu kubwa kabisa kati ya mahekalu ya kuabudu mungu wa mito nchini China. Hekalu hilo limekuwepo kwa miaka 1400, na limeorodheshwa katika urithi wa kitaifa wa utamaduni. Wataalamu wanalisifu hekalu hilo kuwa ni makumbusho ya majengo ya kale ya China. |
Vivutio maarufu vya utalii kwenye sehemu zilizoko kando za Reli ya Qinghai-Tibet 2006/07/03 Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet, China imezinduliwa kuanzia tarehe 1 Julai mwaka huu, reli hiyo imejengwa kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet wenye mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari. |
Maporomoko ya maji ya Huangguoshu 2006/06/19 Maporomoko ya maji ya Huangguoshu yako kwenye sehemu ya vivutio vya Maporomoko ya Huangshuo mkoani Guizhou, kusini magharibi ya China. Katika sehemu hiyo, kuna maporomoko 18 ambayo yanaonekana kwenye uso wa dunia, ambayo yameundwa kuwa kundi kubwa la maporomoko. |
Mji mdogo wa kale uitwao Pingyao na mahoteli mengi yaliyopo mjini humo 2006/06/05 Mji mdogo wa kale uitwao Pingyao mkoani Shanxi, kaskazini ya China ni mji wenye vivutio vingi vya utalii. Mji huo ni mji wa wilaya ya kale unaohifadhiwa kikamilifu zaidi nchini China. |
Hekalu la Famensi 2006/05/22 Katika zaidi ya miaka 3000 iliyopita, miji mkuu ya madola ya kifalme katika enzi 12 za China ya kale ilikuwepo mkoani Shanxi. Mpaka sasa mkoani humo yanahifadhiwa majengo mengi ya zama za kale na mabaki mengi ya utamaduni. Miongoni mwao, Hekalu la Famensi lenye historia zaidi ya miaka 1700 linawavutia sana watalii. |
Hoteli dogo za kitibet mjini Lahsa 2006/04/24 Mji wa Lahsa ulioko kwenye sehemu yenye mwinuko wa mita 3600 kutoka usawa wa bahari, mbali na anga la buluu, na Mto Lahsa wenye maji safi pamoja na mahekalu ya walama ya rangi nyekundu na nyeupe, pia kuna hoteli ndogondogo za kitibet zilizotapakaa mjini Lahsa ambazo zinawavutia watalii wengi. |
Hekalu la Confucius, mnara wa ngoma na ukumbi wa shirikisho la wafanyabiashara wa Guangdong mjini Tianjin 2006/04/03 Mji wa Tianjin uko kusini ya Beijing kwa umbali wa muda wa saa mbili hivi kwa safari ya gari, mji huo umekuwa na historia ya miaka mia sita. Tianjin ni mji wa kale wenye kumbukumbu nyingi za utamaduni, kwa sababu mjini humo watu wanaweza kuona michezo ya aina mbalimbali ya jadi, vitu na majengo mengi ya kale. |
Maporomoko ya maji ya Huangguoshu 2006/03/20 Leo tunawaongoza kwenda kwenye sehemu ya Maporomoko ya maji ya Huangguoshu, ambayo ni moja ya sehemu zenye mandhari nzuri zaidi nchini China. Maporomoko ya Huangguoshu ni ya kipekee duniani, ambayo yanaweza kuguswa na watu kwa mikono. |
Vivutio vya maua ya Also (cymbidium) mjini Guiyang 2006/03/13 Guiyang ni mji mkuu wa mkoa wa Guizhou, mjini humo hakuna baridi kali katika majira ya baridi, na hakuna joto kali katika majira ya joto, hali ya hewa ya huko inafaa sana kwa ukuaji wa maua ya Also. |
Dali, Mji wa kale wenye vivutio 2006/02/27 Katika mkoa wa Yunnan, kusini mwa China, kuna mji mmoja wenye historia ya zaidi ya miaka 600 unaoitwa Dali. Mpaka sasa mji wa Dali kimsingi bado unadumisha mpangilio wake wa kale, mjini humo kuna majengo mengi yaliyojengwa zamani, na wakazi wengi wa mji huo wanafuata desturi na mila za zamani. |