Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
Madhari nzuri ya mkoa wa Si Chuan, Wo Long (5) 2007/01/09
Vivutio vya "Mkoa wa Sichuan, Maskani ya Panda". Katika makala tulizosoma wiki kadhaa zilizopita, tuliwajulisha vivutio vya utalii mkoani Sichuan, leo tunawaletea makala ya 5 yaani makala ya mwisho ya chemsha bongo hiyo, ambapo tutazungumzia wanyama Panda ambao ni alama ya Mkoa wa Sichuan, ambao wanaishi katika hifadhi ya maumbile ya Wolong ililioko umbali wa zaidi ya kilomita 100 kutoka Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan.
Kijiji cha Sanxingdui chenye mambo yasiyofahamika 2006/12/11
Wakati Sehemu ya Sanxingdui ilipoitwa kuwa ni "Kijiji cha Nyota tatu", hakuna mtu aliyeweza kufikiri kuwa, mkulima Yan alipokuwa akilima mashamba angegundua mabaki ya Sehemu ya Sanxingdui, ugunduzi huo uliwashangaza watu, baadaye watafiti walifanya kazi za kufukua na kufanya utafiti kwa miongo kadhaa, wakathibitisha kuwa sehemu ya Mabaki ya Kijiji cha Sanxingdui ilikuwa sehemu ulipokuwa mji mkuu wa Dola la Shu la kale
Kijiji cha kale cha Liukeng mkoani Jiangxi, China 2006/11/20
Kijiji cha kale cha Liukeng kinasifiwa na wataalamu wa China kuwa ni Kijiji cha kale cha kwanza cha China, ambacho kiko katika Wilaya ya Lean, mjini Wuzhou mkoani Jiangxi. Kijiji hicho kilianzishwa katika karne ya 10, na sasa kimekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1000. Eneo la kijiji hicho ni kilomita 4 hivi, ambapo kuna majengo zaidi ya 500 yaliyojengwa katika enzi mbalimbali.
Shughuli za utalii kwenye sehemu za vijijini nchini China zapiga hatua kubwa  2006/10/30
Maendeleo ya soko la utalii kwenye sehemu ya vijijini nchini China bado yako katika kipindi cha mwanzo, lakini soko hilo lina nafasi kubwa za uendelezaji na biashara katika siku za baadaye
Mapango ya mawe ya chokaa ya Diaoshuihu 2006/10/09
Tukifunga safari kutoka Changchun, mji mkuu wa mkoa wa Jilin, baada ya muda wa saa moja na nusu tu, tutafika kwenye bustani ya misitu ya taifa ya Diaoshuihu ya Changchun. Katika bustani hiyo kuna mapango ya mawe ya chokaa.
Maduka maarufu mjini Beijing 2006/09/25
Mji wa Beijing ni mji mkuu wa China wenye historia ndefu, mbali na vivutio kadha wa kadha vya utalii, pia kuna maduka mengi maarufu yaliyoanzishwa tangu zamani sana, ambayo yameonesha historia na hadithi za kuvutia kuhusu Mji wa Beijing
Ziwa la Baiyangdian  2006/09/11
Ziwa la Baiyangdian liko katika Wilaya ya Anxin mkoani Hebei, ambayo iko kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 160 kutoka Beijing. Eneo la ziwa hilo ni kilomita 366 za mraba, ambapo kuna maziwa 143. 
Mapango ya mawe wilayani Longyou 2006/08/28
Leo tunawaongoza kwenda Wilaya ya Longyou kutembelea mapango ya mawe. Wilaya ya Longyou iko mkoani Zhejiang, mashariki ya China. Zaidi ya miaka 10 iliyopita mapango mengi ya mawe yaliyoko chini ya ardhi yaligunduliwa katika wilaya hiyo
Mapango ya Qianfodong 2006/08/14
Mapango ya Mogao yanaitwa pia ni Mapango ya Qianfodong, maana yake ya kichina ni mapango elfu moja ya Buddha, mapango hayo ni mabaki ya utamaduni wa dini ya kibudha yanayojulikana duniani.
Jumba la makumbusho la Henan  2006/07/31
Mkoa wa Henan ulioko katikati ya China ni moja ya chimbuko la ustaarabu wa zama za kale za China. Historia ndefu ya mkoa huo imeuachia mali nyingi za urithi wa historia na utamaduni.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11