Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
Mlima Wudang  2004/09/01
Mlima Wudang unajulikana kwa mandhari yake nzuri na utamaduni wake mkubwa. Ni sehemu yenye mahekalu mengi ya dini ya Dao, dini ambayo iko nchini China peke yake. Mwaka 1994 mlima Wudang uliorodheshwa kwenye kumbukumbu za urithi wa dunia.
Sehemu ya Kivutio ya Jiouzhaigou nchini China  2004/08/23
Sehemu ya kivutio ya Jiouzhaigou inajulikana duniani kwa mandhari yake nzuri ya kimaumbile. Sehemu hiyo iko kusini magharibi mwa China. Mwaka 1992 iliwekwa kwenye orodha ya kumbukumbu za urithi wa dunia, na mwaka 1997 iliorodheshwa katika "hifadhi ya viumbe ya dunia".
Vivutio vya mandhari ya milima na mito mkoani Zhejiang  2004/08/16
 Mkoa wa Zhejiang uko kwenye pwani ya mashariki ya China. Mkoa huo una vivutio vingi vya utalii, kama vile Ziwa Xihu mjini Hangzhou, mji mdogo unaopendeza wa wilaya wa Xitang, na mji wa Shaoxin wenye mito mingi yenye mitumbwi yenye vifuniko ya rangi nyeusi inayopita mara kwa mara. Aidha, mkoani humo kuna vivutio 11 vya ngazi ya kitaifa kama vile Ziwa Qiandao, yaani Ziwa la visiwa elfu moja kwa maana ya kichina, Mlima Yandang, Mlima Putuo, mkoa wa Zhejiang kwa kweli ni sehemu yenye vivutio vingi vya utalii.
Hifadhi ya paa ya Dafeng  2004/08/12
Jua kubwa linaangaza mbali juu ya vichaka. Ukungu unaelea kwenye mwambao wa Bahari Huanghai. Kundi la paa waitwao David's deer wananyemelea bwawa la maji. Ghafula ulisikika mshindo wa kutembea kwa watu, paa wote walishituka na kukimbilia vichakani. Hii ndiyo hifadhi ya paa ya Dafeng jimboni Jiangsu, yenye ukubwa wa hekta 1000.
Tusafiri kuelekea Kanas 2004/08/09
Mkoa ujiendeshao wa Xinjiang Uygur 2004/08/02
Nchini China watu wengi wakiutaja mkoa ujiendeshao wa Xinjiang Uygur, magharibi ya China hupata picha mkoa huo, ambao uko katika sehemu ya jangwa kubwa ambapo kuna zabibu tamu na wasichana warembo na wenye uchangamfu.
Mlima wa kwanza wa ajabu na hatari duniani  2004/07/30
Utamaduni wa Mlima Huashan ni tele na wa miaka mingi. Katika kitabu cha historia kiitwacho "kumbukumbu ya historia" imeandikwa kwamba Wafalme Huangdi, Yao na Shun, waliwahi kutalii mlima huo.
Safari katika mji mdogo wa Wuzhen 2004/07/26
Mji mdogo wa Wuzhen uko mashariki ya China, muundo wa mji huo unaonekana kama msalaba. Kama ilivyo ya miji mingi ya kusini mwa Mto Changjiang, mto unapita kufuata mji huo na matawi yake makubwa na madogo yanafika kila mahali. Barabara zote zinazotanda kuelekea pande zote nne si ndefu. Kutoka mashariki hadi magharibi ni kilomita 3.75 na kutoka kusini hadi kaskazini ni fupi zaidi.
Safari kwenye Ghuba ya Sanniang mjini Qingzhou 2004/07/19
Ghuba ya Sanniang ya  Qingzhou iko katika mkoa ujiendeshao wa kabila la wazhuan wa Guagxi, kusini magharibi ya China.
Daraja la Longnao  2004/07/15
Daraja la Longnao katika mto Jiuqu, Wilaya ya Luxian, ambalo lipo kusini mwa Jimbo la Sichuan lilijengwa katika utawala wa Mfalme wa Hongwu, Enzi ya Ming (mwaka 1368-1398).
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11