Baraza jipya la mawaziri latangazwa Hispania
Waziri mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy, ametangaza baraza jipya la mawaziri kumi na watatu.
Bwana Rajoy, alimtaja Luis de Guindos kama waziri wa uchumi wakati naibu waziri mkuu Soraya Saenz de Santamaria atachukua jukumu la uhusiano wa Madrid na mamlaka ya kikanda ya mfalme.
Waziri mkuu Rajoy, alishinda kura ya imani mwishoni mwa wiki, iliyomwezesha kuingia madarakani baada ya chaguzi mbili za pamoja za uchaguzi mkuu, na miezi kumi ya kupooza kisiasa.
Baraza hilo jipya la mawaziri lilikutana Ijumaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |