Burudi yatishia kuondoa wanajeshi wake Somalia
Serikali ya Burundi imetishia kuondoa askari wake wa kulinda amani nchini Somalia katika kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM iwapo umoja wa ulaya, mfadhili mkuu wa kikosi hicho, hauto rejelea uamuzi wake wa kutopitisha mishahara ya askari hao mikononi mwa serikali.
Burundi ina wanajeshi zaidi ya elfu tano mia tano nchini Somalia, ikiwa kwenye nafasi ya pili baada ya Uganda , kwa nchi zilizo tuma vikosi vya kulinda amani katika nchi hiyo iliopo upembezoni mwa Afrika.
Waziri wa ulinzi Emmanuel Ntahomvukiye aliliambia bunge kuwa wanajeshi hawajapata mishahara yao ya kila mwezi ya dola 800 kutoka kwa muungano wa ulya kwa muda wa miezi kumi.
Burundi ndiyo nchi ya pili inayochangia wanajeshi wengi zaidi katika kikosi cha AU kinachopigana na al-Shabab nchini Somalia
Wadadisi wanasema serikali ya Burundi imeamua kusema hivo baada ya kuona kwamba Umoja wa Ulaya, hasa Ubelgiji imeendelea kushikilia uamuzi wa kutopitisha mishahara ya askari wa Burundi waliotumwa nchini Somalia mikononi mwa serikali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |