Kituo cha jeshi la majini la Marekani huko Nagasaki, Japan chafungwa baada ya kuripotiwa ufyatuaji wa risasi
Kituo cha jeshi la majini la Marekani huko Nagasaki, Japan kilifungwa leo asubuhi kwa saa moja kutokana na ripoti za ufyatuaji wa risasi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Facebook wa kituo hicho, ufyatuaji risasi uliripotiwa saa tatu na nusu asubuhi kwa saa za huko katika jengo moja lililoko katika kituo hicho, ambapo watu waliokuwa ndani ya jengo hilo waliondolewa, huku idara za usalama na zimamoto zikikagua jengo hilo.
Habari nyingine ziansema, hakuna uthibitisho wowote kuwa risasi zilifyatuliwa au mshambuliaji kupatikana, wala majeruhi kuripotiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |