Sudan Kusini yawakamata watu 17 waliowabaka wafanyakazi wa kutoa msaada
Serikali ya Sudan Kusini imethibitisha kukamatwa kwa watu 17 wakiwemo wanajeshi kwa kuhusiana na kuwabaka wafanyakazi wa kutoa msaada wakati wa mapambano kati ya jeshi la serikali na kundi la upinzani yaliyotokea tarehe 11 Julai huko Juba.
Naibu waziri wa sheria wa nchi hiyo Bw. Martinson Oturomoi anayeongoza tume ya uchunguzi wa tukio hilo, amesema waathirika na mashuhuda waliohojiwa wamethibitisha kuwa watu hao waliwabaka wafanyakazi wa kutoa msaada, na kupora misaada ya wakimbizi.
Tume hiyo inapendekeza kuanzisha mara moja mahakama maalumu ili kuwahukumu watuhumiwa hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |