Polisi mmoja auawa katika tukio la ufyatuaji risasi Ufaransa
Polisi mmoja ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi lililotokea jana jioni katika mtaa wa Champs Elysees mjini Paris, Ufaransa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa Bw. Pierre-Henry Brandet amesema maofisa wa polisi walilengwa kwa makusudi, na mshambuliaji ameuawa kwa kupigwa risasi.
Shuhuda amesema, mshambuliaji aliyekuwa na bunduki alitoka nje ya gari na kuwafyatulia risasi polisi na kuanza kukimbia na kuwajeruhi wengine wawili kabla ya kuuawa na polisi.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa ameitisha mkutano wa ulinzi, na alisema anaamini kuwa hili ni shambulizi la kigaidi, na kuahidi kuchukua hatua madhubuti za kiusalama wakati wa uchaguzi wa urais utakaoanza jumapili.
Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |