Mahmoud Ahmadinejad azuiwa kuwania urais Iran
Rais wa zamani Mahmoud Ahmadinejad amezuiwa kuwania urais na jopoi la usimamizi wa masuala ya uchaguzi la serikali.
Rais wa Iran Hassan Rouhani na mwanasiasa Ebrahim Raisi wameidhinishwa kuwania uchaguzi wa urais mwezi ujao nchini humo, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Mshirika wa karibu wa Ahmadinejad Hamid Baghaie pia amezuiwa kugombea urais.
Orodha kamili ya wagombea kwenye uchaguzi huo wa tarehe 19 Mei itatangazwa 27 Aprili.
Wagombea zaidi ya 1,600 walitaka kuwania lakini ni sita pekee ambao walichaguliwa na Baraza Kuu la Walinzi.
Kuidhinishwa kwa Bw Rouhani na Bw Raisi kunatarajiwa kusababisha mvutano mkali wa kisiasa kati ya kambi zao mbili.
Bw Rouhani alichaguliwa kwa kura nyingi mwaka 2013, ambapo aliahidi kufikisha kikomo kutengwa kwa taifa hilo kidiplomasia katika jamii ya kimataifa na kuhakikisha uhuru zaidi wa kijamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |