Waziri mkuu wa Uingereza atangaza kufanya uchaguzi mkuu mapema kuliko ilivyopangwa
Waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amesema Uingereza itafanya uchaguzi mkuu tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu, ikiwa ni mapema kabla ya ilivyopangwa awali, ili kutoa urahisi kwa serikali yake kufanya mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu kuanza mchakato wa kujitoa kwenye Umoja huo.
Bi. May amesema, lengo la uamuzi huo ni kulinda vizuri zaidi maslahi ya Uingereza.
Tarehe 29 mwezi uliopita, Bi. May alitangaza kuzindua rasmi utaratibu wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, na mara utaratibu huo ukianza rasmi, Uingereza italazimika kukamilisha mazungumzo ndani ya miaka miwili.
Kutokana na sheria ya Uingereza, muda wa serikali ya awamu hiyo kuwa madarakani utamalizika mwaka 2020, hata hivyo kufanya uchaguzi mkuu mapema bado kunahitaji kupitishwa na bunge la Uingereza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |