Marekani yafikiria kuirudisha Korea Kaskazini kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson amesema Marekani inafikiria hatua za kuishinikiza Korea Kaskazini ikiwemo kuirudisha nchi hiyo kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Mapema mwezi huu, baraza la chini la bunge la Marekani lilipitisha uamuzi wa kuiagiza wizara ya mambo ya nje iamue kama itaitangaza Korea Kaskazini kuwa nchi inayofadhili ugaidi, lakini uamuzi huo haujapigiwa kura kwenye Baraza la juu.
Russia imezitaka pande mbalimbali zijizuie katika suala la Korea Kaskazini na kutatua suala hilo kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia chini ya mfumo wa kimataifa. Na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema China inafuatilia kwa karibu hali ya Korea Kaskazini, na inapinga kauli na vitendo vyovyote vya uchochezi
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |