Uturuki yarefusha hali ya dharura kwa miezi mitatu zaidi
Naibu waziri mkuu wa Uturuki Bw Numan Kurtulmus amesema hali ya dharura nchini humo itarefushwa kwa muda wa miezi mitatu zaidi.
Bw Kurtulmus amesema bunge la Uturuki limeidhinisha uamuzi huo, na kusema lengo lake ni kupambana na matishio ya ugaidi, hasa dhidi ya Kundi la kigaidi Fetullah FETO, lililofanya jaribio la mapinduzi tarehe 15 Julai mwaka jana.
Ikulu ya Ufaransa imeitaka serikali ya Uturuki ifanye mazungumzo na pande zote nchini humo. Ufaransa imesema itafuatilia matokeo ya ripoti ya tathmini itakayotolewa na bunge la Ulaya na Shirika la usalama na ushirikiano la Ulaya OSCE, kuhusu upigaji kura za maoni nchini Uturuki.
Ikulu ya Marekani pia imesema kabla ya jopo la waangalizi wa kimataifa kutoa ripoti kuhusu kura za maoni nchini Uturuki, Marekani haitatoa maoni yake kuhusu matokeo ya kura hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |