Iran na Russia zashirikiana kujenga vituo viwili vya umeme vya nyuklia
Waziri wa nishati wa Iran Bw Hamid Chitchian amesema Iran itashirikiana na Russia na kujenga vituo viwili vya umeme vya nyuklia nchini humo.
Bw Chitchian amesema Shirika la nishati ya Atomiki la Iran AEOI limesaini makubaliano na Russia kuhusu ujenzi wa vituo viwili vya nyuklia vyenye uwezo wa kuzalisha megawati 1,000 za umeme. Kiongozi wa shirika hilo Bw Ali Akbar Salehi amesema kwamba ujenzi wa vituo hivyo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ameongeza kuwa wizara ya nishati ya Iran inashirikiana na serikali ya Russia katika mradi mwingine wa kituo cha kuzalisha umeme cha megawati 1,400 mkoani Hormozgan, karibu na ghuba ya uajemi, na mradi huo umeanza kujengwa.
Mwezi Februari mwaka huu waziri wa nishati wa Russia Bw Alexander Novak alisisitiza kuwa Russia inapenda kusaini makubaliano na Iran, na kuisaidia kujenga vituo vya kuzalisha umeme.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |