Afrika Kusini ilistahili kumkamata Bashir
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeamua kuwa Afrika Kusini, ilifanya makosa kwa kutomkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati alifanya ziara nchini humo mwaka 2015
Ilisema kuwa Bashir hakuwa na kinga ya kidiplomasia na hivyo angekamywa na kukabidhiwa kwa mkuu wa mashtaka kwa wa ICC kufuatia madai ya kuhusika kwenye mzozo wa jimbo la Darfur.
Serikali ya Rais Jacob Zuma, imesema kuwa masharti ya ICC yanaenda kinyume na sheria za nchi na kuwa imeanzisha mchakato wa kuondoka kutoka uanachama wa ICC, hatua ambayo makundi ya haki yanapinga.
Mahakama ya juu pia imeamua kuwa serikali imeenda kinyume na katiba kujiondoa kutoka ICC baada ya kushindwa kuomba ushauri wa bunge.
Lakini nalo bunge la Afrika Kusini jana lilipinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, kuhusu Afrika Kusini kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa mahakama hiyo na kumkamata Rais Omar Al Bashir alipokuwa nchini Afrika Kusini mwezi juni mwaka 2015.
Msemaji wa kamati ya ushirikiano wa kimataifa ya bunge la Afrika Kusini Bw Shiphosezwe Masango, amesema inatakiwa kukumbwa kuwa Rais Al Bashir hakwenda Afrika Kusini kwa mwaliko wa serikali ya Afrika Kusini, bali alikuwa anahudhuria mkutano wa umoja wa Afrika.
Wiki hii chama tawala cha ANC, kilisema kuwa kina mpango ya kuiondoa nchi hiyo kutoka mahaka ya ICC.
Hii ni sehemu ya kampeni kubwa kutoka kwa baadhi ya nchi za kiafrika zinazodai kuwa ICC inawalenga viongozi wa bara la Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |