Syria yaishutumu Uturuki kuweka kituo cha kijeshi kaskazini mwa Syria
Wizara ya mambo ya nje ya Syria jana imesema kitendo cha Uturuki kuweka kituo cha kijeshi kaskazini mwa Syria ni kitendo cha uvamizi.
Wizara hiyo imewasilisha barua ya malalamiko kwa mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katibu mkuu wa umoja huo, ikitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya kitendo hicho cha Uturuki.
Barua hiyo imesema Uturuki imefanya mashambulizi dhidi ya wilaya ya Azaz na Kipling mkoani Aleppo hivi karibuni, kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya kiamatifa, maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Matiafa na Katiba ya Umoja wa Mataifa, na pia ni tishio kubwa kwa usalama na utulivu wa kikanda na wa kimataifa.
Mwezi uliopita rais Recep Tayyip Erdogan Uturuki alisema Uturuki itarejesha opresheni za kijeshi kaskazini mwa Syria kama Kundi la Wakurdi la Syria likiishambulia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |