Watu 80 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Jamhuri ya Afrika ya Kati
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lori moja la mizigo limesababisha vifo vya zaidi ya watu 80, wengi wakiwa wachuuzi waliokuwa wakielekea sokoni mjini Bambari.
Maafisa wa ualama wa barabarani wamelaumiwa kwa kutochukua hatua kuzuia ukiukwaji huo wa sheria za barabarani.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema lori hilo lilikuwa limebeba watu wengi na kujazwa mizigo kupindukia huku likiendeshwa kwa mwendo wa kasi wakati lilipopenduka.
Ajali kama hii zimekua zikitokea, katika za Afrika ya Kati na Magharibi, hasa nchini Jmhuri ya Afrika Kati ambapo polisi inanyooshewa kidole kwa kujihusisha na rushwa ya kupindukia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |