• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (1 Juni-7 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-07-10 10:43:20

    Tanzania yaiomba DRC kusaidia raia wake 21 waliotekwa nyara waachiwe

    Serikali ya Tanzania imeiomba serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC kuwasaidia raia wake 21 waliotekwa nyara mwezi uliopita na waasi wa Mai Mai katika misitu ya nchi hiyo.

    Madereva hao wa malori wa Tanzania walitekwa nyara Juni 19 pamoja na madereva watatu wa Kenya.

    Walitekwa katika eneo la Lulimba umbali wa kilomita 100 kutoka wilaya ya Baraka iliyoko Kivu Kusini, wakati walipokuwa wakielekea kwenye mgodi wa dhahabu wa Namoyo mkoani Mainiema. Waasi hao pia walipora mali zao.

    Ofisa habari wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Bibi Mindi Kasiga amesema, ingawa madereva hao wameachiwa huru, lakini wako katika hali ngumu kwa kuwa hawawezi kuondoka katika eneo hilo bila ulinzi.

    Bibi Kasiga ameongeza kuwa serikali ya nchi hiyo itafanya chini juu kuhakikisha madereva hao wote wanaokolewa salama.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako