Mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika na Umoja wa Ulaya waanzisha mpango mpya wa uhamiaji mjini Rome
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuhusu mpango mpya wa kusimamia uhamiaji, ili kuwapa watu njia ya kisheria ya uhamiaji badala ya kuwatafuta watu wanaosafirisha watu kwa njia za magendo.
Kwenye mkutano huo ulioendeshwa chini ya uenyekiti wa Italia, mawaziri wamekubaliana kuchukua hatua za kuwasaidia wahamiaji na watalii walio kwenye nchi za mpito, na kuboresha njia ya uhamiaji wa kawaida.
Nchi zilizoshiriki pia zimekubali kulisaidia shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR kuhakikisha njia zenye ufanisi na salama za kuomba hifadhi, na kutoa njia mbadala za kisheria kwa wakimbizi wanaokwama njiani.
Utaratibu huo mpya unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Februari mwaka kesho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |