Somalia kuwakagua wapiganaji waliojitenga na kundi la Al-Shabaab
Idara za usalama za Somalia wiki hii zimeanzisha mpango wa kuwakagua wapiganaji waliojitenga na kundi la Al-Shabaab na kutaka kurudi katika jamii.
Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM uliofungwa mjini Mogadishu, umepitia taratibu za utendaji na ujenzi wa uwezo wa idara ya ujasusi na usalama ya taifa NISA kwa ajili ya kuwakagua wapiganaji hao.
Kamanda wa polisi wa UNSOM Bw. Christoph Buik amesema, idara za usalama kama vile idara ya NISA ni nguzo ya mpango wa kushughulikia suala hilo, ambao ni sehemu muhimu ya mpango wa taifa wa kuwashughulikia wapiganaji wanaojitenga na kundi la Al-Shabaab.
Mkutano huo pia umejadili njia za kupambana na ugaidi na kuhakikisha kuwa wapiganaji wanaojitenga na kundi la Al-Shabaab na kutaka kujiunga na jamii wanapata uungaji mkono wa lazima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |