Marais wa China na Korea Kaskazini wafanya mazungumzo
Rais Xi Jinping wa China na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ambaye yupo ziarani nchini China wamefanya mazungumzo hapa Beijing wakibadilishana maoni kwa kina kuhusu uhusiano kati ya pande hizo mbili, na masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja na nchi zao.
Viongozi hao wamekubaliana kufanya juhudi za pamoja kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya katika zama mpya, kuendelea kusukuma mbele mchakato wa ufumbuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu Peninsula ya Korea, kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango kwa ajili ya amani, utulivu, ustawi na maendeleo ya kikanda na dunia nzima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |