• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 5-January 11)

    (GMT+08:00) 2019-01-11 18:56:22

    Rais wa Nigeria aahidi uchaguzi huru na wa haki

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameahidi kuwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao utakuwa wa kuaminika, huru na wa haki.

    Akihutubia mkutano wa chama tawala cha APC mjini Abuja, Rais Buhari amesema uchaguzi wa kuaminika, huru na wa haki ni msingi wa utulivu wa kisiasa na amani kwa nchi yoyote Ameongeza kuwa tangu mwaka 2015, tume huru ya uchaguzi imeendesha chaguzi za kuaminika kwenye majimbo 195 nchini Nigeria, ambazo zimethibitishwa kuwa bora.

    Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi ya Nigeria Bw Mahmood Yakubu, amesema watu zaidi ya milioni 84 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao, idadi ambayo ni asilimia 42 ya wananchi wote, na imeongezeka kwa watu milioni 15.2 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2015.

    Buhari amesema ana uhakika wa kushinda muhula wa pili, wakati wa Uchaguzi Mkuu unaopangwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu.

    Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, ameendelea na kampeni nchini humo kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 16 mwezi Februari.

    Wagombea 73 wanawania urais, lakini ushindani unatarajiwa kuwa kati ya Buhari na mgombea wa chama kikuu cha upinzani PDP Atiku Abubakar.

    Buhari, anawania muhula wa pili wa miaka minne, kuongoza taifa hilo la Afrika Magharibi lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, huku ujumbe wake wa kampeni ukiwa ni kuendeleza vita dhidi ya ufisadi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako