Watu 171 wakamatwa kutokana na vurugu za kikabila Ethiopia
Ethiopia imetanganza kuwakamata watu 171 kutokana na tuhuma za kuhusika na vurugu za kikabila katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.
Shirika la utangazaji la taifa la Ethiopia limetoa ripoti ikisema, kituo cha jeshi la Ethiopia kilichopewa jukumu la kulinda usalama wa maeneo ya mpakani ya Benishangul Gumuz na majimbo ya kikanda ya Oromia yenye vurugu, kimewakamata watuhumiwa hao katika siku kadhaa zilizopita.
Ripoti imeongeza kuwa jumla ya bunduki 49 aina ya Kalashnikov, bastola 71, magobole 15, mishale 215, magari 9, pikipiki 3 na maelfu ya risasi zimekamatwa pamoja na watuhumiwa hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |