Bunge la Marekani lapitisha muswada kumaliza kufungwa kwa serikali
Baraza la chini la bunge la Marekani limepitisha mpango wa matumizi ya fedha ambao utaweza kumaliza kufungwa kwa muda kwa serikali, wakati ikulu ya Marekani ikitishia kuzuia mpango huo.
Wabunge wa chama cha Democratic cha Marekani wanaodhibiti baraza hilo wamepitisha miswada inayofadhili idara za jimbo, biashara, kilimo, nguvu kazi, fedha n.k. hadi Septemba 30 ambayo ni mwisho wa mwaka huu wa kifedha.
Hata hivyo, miswada hiyo inaonekana kushindwa baada ya kuwasilishwa katika baraza la juu la bunge wakati ikulu ya Marekani ikitishia kuizuia kutokana kutotoa fedha kwa ujenzi wa ukuta -uliopo katika mpaka wa Marekani na Mexico ulioahidiwa na rais Donald Trump kwa muda mrefu.
Ikulu imesema kabla ya upigaji kura huo washauri wa rais Trump watapendekeza rais kuzuia muswada huo kama fedha ya ujenzi wa ukuta wa mpakani hazitatengwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |