Kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Syria kwatajwa kutoathiri mapambano ya dhidi ya kundi la IS
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ambaye ambaye amefanya ziara wiki hii nchini Jordan, amesema uamuzi wa Marekani kuondoa jeshi lake nchini Syria hautaathiri uwezo wa muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi la IS.
Bw. Pompeo amesema hayo katika mkutano na wanahabari na mwezake wa Jordan Bw. Ayman Safadi, huku akisema uamuzi wa Marekani kuondoa jeshi kutoka Syria hautaathiri uwezo wa kutimiza lengo hilo.
Ameongeza kuwa katika siku zijazo Marekani itaongeza juhudi za kidiplomasia na kibiashara kuweka shinikizo halisi dhidi ya Iran, ili kutimiza lengo lililowawekea mwezi wa Mei.
Habari nyingine zinasema wapiganaji wenye uhusiano na makundi ya al-Qaida na IS wamefanya mashambulizi kwa nyakati tofauti dhidi ya vikosi vya SDF mashariki na kaskazini magharibi mwa Syria, na kusababisha vifo vya askari 23 wa SDF na wengine wengi kujeruhiwa.
Awali rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake Emmanuel Macron wa Ufaransa walijadiliana kwa njia ya simu kuhusu suala la Syria.
Msemaji wa ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesema, rais Trump na rais Macron wamejadiliana kuhusu hali ya sasa nchini Syria, ikiwemo mapambano dhidi ya kundi la IS na mpango wa jeshi la Marekani kuondoka Syria.
Habari zinasema, Marekani itaondoa jeshi lake lote nchini Syria baada ya kutathmini kwa makini na kufanya uratibu na pande mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |