Jumuiya ya Afrika Mashariki yatishia Burundi kuifuta uanachama wa jumuiya
Bunge la Afrika Mashariki limepitisha mswada wa kutaka kuifukuza Burundi kutoka kwenye uanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kutolipa madeni ya michango yake ya 2016-2017, 2017-2018, na 2018-2019.
Hii si mara ya kwanza kwa Burundi kukumbwa na tishio kama hili, lakini serikali ya Burundi imelalamika kuwa habari kuhusu deni lake kwa jumuiya ya Afrika Mashariki hazitolewi kwa haki.
Burundi sio nchi pekee inayodaiwa ada ya uanachama, nchi nyingine iliyotajwa kuwa na deni ni Sudan Kusini, na hata nchi zilizolipa michango wakati mwingine huchelewa kulipa michango hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |