Viongozi wa AU jumanne wiki hii waanza mazungumzo mapya kuhusu bwawa la GERD la Mto Nile
Viongozi wa nchi za Afrika jumanne walifanya mkutano kuhusu mvutano wa muda mrefu kati ya Misri, Ethiopia na Sudan juu ya bwawa la Grand Ethiopia Renaissance (GERD) la Ethiopia lililoko kwenye mto Nile.
Mkutano huo uliitishwa Umoja wa Afrika (AU), chini ya uenyekiti wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Bwawa la GERD limekuwa chanzo cha mvutano katika bonde la Mto wa Nile tangu Ethiopia ilipozindua mradi huo mnamo 2011. Sudan na Misri zinaona bwawa hilo ni tishio kwa mgao wa maji, wakati Ethiopia inaliona ni muhimu katika kuzalisha umeme kwa ajili ya maendeleo yake. Mpaka sasa raundi tatu za mazungumzo hayo zimefanyika bila kuwa na mafanikio yoyote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |