Eneo la Biashara Huria barani Afrika kuleta fursa mpya kwa ushirikiano wa China na Afrika
Mtaalam wa Ethiopia Gedio Jalata amesema, Eneo la Biashara Huria barani Afrika (AfCFTA) litaleta fursa mpya kwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika
Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, Jalata amesema AfCFTA inataka mawasiliano imara ya miundombinu katika bara la Afrika, na msaada wa China utahitajika sana. Amesema kasi ya ujenzi wa miundombinu barani Afrika ni ndogo, na nchi kama China ina uzoefu mkubwa katika ujenzi wa miundombinu, na inaweza kuzisaidia nchi za Afrika kujenga barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege.
Jalata amesema hivi sasa thamani ya biashara kati ya nchi za Afrika inachukua asilimia 17 tu ya thamani ya jumla ya biashara ya bara hiyo, na sababu kuu ni hali duni ya mawasiliano ya miundombinu kati ya nchi za Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |