Uchaguzi mkuu wa Tanzania kufanyika Oktoba 28
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania jumatano (NEC) ilitangaza kuwa, uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika tarehe 28, mwezi Oktoba mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na mwenykiti wa NEC BW. Semistoeles Kaijage imesema, Agosti 25, Tume hiyo itapitisha wagombea wa urais, wabunge na madiwani walioteuliwa na vyama vyao.
Taarifa hiyo pia imesema, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 26, mwezi ujao hadi tarehe 27, mwezi Oktoba, siku moja kabla ya uchaguzi.
Tume hiyo imesema, Watanzania milioni 29 wamejiandikisha kushiriki uchaguzi wa mwaka huu, ikilinganishwa na Watanzania milioni 23 waliojiandikishwa mwaka 2015.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |