Kenya yapokea vifaa ya kupambana na virusi vya Corona kutoka China
Kenya imepokea shehena ya vifaa tiba vya kupambana na virusi vya Corona vilivyotolewa na serikali ya China kupitia Jumuiya ya Wake wa Marais wa Afrika kwa ajili ya Maendeleo (OAFLAD) ili kuwasaidia wanawake na watoto kupambana na virusi vya Corona.
Ubalozi wa China nchini Kenya ulipewa vifaa hivyo na mke wa rais wa China Bi. Peng Liyuan, na kuvikabidhi kwa Angella Githere-Langat, Mratibu wa Mfuko wa Beyond Zero wa Mama Margaret Kenyatta, mke wa rais wa Kenya.
Bi. Githere-Langat amesema msaada huo utasaidia katika juhudi za mke wa rais wa Kenya katika kuwalinda wanawake, watoto, wazee na makundi mengine yaliyo hatarini dhidi ya janga la virusi vya Corona.
Kaimu balozi wa China nchini Kenya Zhao Xiyuan amesema, msaada huo unaonyesha jinsi mke wa rais wa China Peng Liyuan anavyojali afya na maendeleo ya wanawake na watoto wa Kenya, na pia urafiki kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |